Omog amesema kucheza fainali ya FA na timu ya Mbao FC kuna presha kutakuwa na presha kubwa tofauti na kama wangecheza na Yanga

Kocha mkuu wa Simba Joseph Omog , amesema kucheza fainali ya FA na timu ya Mbao FC kuna presha kutakuwa na presha kubwa tofauti na kama wangecheza na Yanga.
Omog ameiambia Goal, pamoja na mchezo huo kupigwa uwanja wa Taifa Dar es Salaam, wanalazimika kucheza kwa tahadhari kwani hata kubwa kwani wakifanya mzaha wanaweza wakapoteza nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa.
"Hatupo katika nafasi nzuri ya kubeba ubingwa kwa hiyo nilazima tucheze kwa nguvu na kushinda mapema vinginevyo tunaweza kuharibikiwa siku ya mwisho na kupoteza nafasi ya michuano ya kimataifa," amesema Omog.
Kocha huyo raia wa Cameroon amesema Mbao ni timu nzuri na yenye kutoa upinZani sehemu yoyote wanapocheza hivyo nilazima waachezaji wake wapambane kwenye mechi ya fainali kama wanataka kucheza michuano ya kimataifa.
Amesema amejifunza mambo mengi kwa timu hiyo aliyocheza nayo wiki mbili zilizopita na kutanguliwa kufungwa mabao mawili hivyo amekiri mchezo utakuwa mgumu sana kwao.
"Tutacheza kwa presha tukijua ikitokea tumepoteza hatuna nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa wenzetu Mbao hawana presha kubwa kama ilivyo kwetu kwasababu sidhani kama wao malengo yao ni kushiriki michuano ya kimataifa kutokana na uchanga wao," amesema.
Aidha kocha huyo amesema kabla ya mchezo wa fainali ataendelea kuwafatilia Mbao FC, katika mechi zao za ligi ya Vodacom ili kujua mbinu zao wanazotumia na kuziwekea mikakati ya kuzidhibiti.
Simba inalazimika kushinda mechi hiyo ya faibali ili kushiriki michuano ya Kombe la Shirikiso Afrika kwani enapo itafungwa na Mbao na huku ikikosa taji la ligi ya Vodacom itakuwa kazi bure kwao.
Simba
Mbao
Tous les commentaires