Farid amefunga magoli matano katika mechi 12 alizoichezea timu hiyo huku akiwa amepiga pasi za mwisho sita

Mtanzania anaecheza soka la kulipwa nchini Hispania Farid Musa, ameendelea kufanya vizuri kwenye klabu yake ya Tenerife B inayocheza ligi ya vijana.
Farid amefunga magoli matano (5) katika mechi 12 alizoichezea timu hiyo huku akiwa amepiga pasi za mwisho sita (6).
Nyota huyu ambaye anaichezea pia Taifa Stars alisajiliwa na Tenerife akitokea Azam FC lakini alipelekwa kwenye kikosi cha vijana ili kujifunza aina ya soka pamoja na mifumo mbalimbali inayotumiwa na klabu hiyo kabla ya kuanza kucheza kwenye kikosi cha wakubwa.
“Nimeanza kupata nafasi kwenye kikosi B lengo likiwa kufundishwa aina ya soka lao na mifumo wanayoitumia ili nikianza kucheza kwenye timu ya wakubwa kusiwe na kazi kubwa ya kuelekezwa nini natakiwa kufanya,” alisema Farid alipoitwa kwenye kikosi cha Stars kilichocheza mechi mbili za kirafiki za kimataifa dhidi ya Botswana na Burundi.
Mtanzania huyo amekuwa akionyesha jitihada za pekee huko ughaibuni sambamba na Mbwana Samatta anayekipiga Genk Ubelgiji.
Azam
Kagera Sugar
Tutti i commenti