Banda amesema yupo kwenye mazoezi makali akijiandaa kuanza kwenye kikosi cha kwanza kitakachocheza mechi ya fainali ya Kombe la FA

Mlinzi wa kati wa Simba Abdi Banda amesema yupo kwenye mazoezi makali akijiandaa kuanza kwenye kikosi cha kwanza kitakachocheza mechi ya fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC Mei 28 Dododma.
Band ameiambia Goal, ni mchezo muhimu ambao angependa kuwa miongoni mwa wachezaji 11 watakaoanza kwenye kikosi cha Simba ndiyo maana amekuwa akijifua ili kumshawishi kocha ampe nafasi.
“Ni mchezo mkubwa wenye kuweka kumbukumbu nzuri kwasababu mshindi atabeba kombe na pia ataiwakilisha nchini kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho hivyo ningependa kuanza kikosi cha kwanza na kuitumia vizuri nafasi hiyo kwa kuisaidia timu yangu na ikiwezekana kufunga bao,”amesema Banda.
Beki huyo ambaye hivikaribuni aliachiwa huru na Kamani ya Nidhamu na Sheria za Wachezaji baada ya kusimamishwa mechi mbili na Kamati ya saa 72, kutokana na kumpiga ngumi Nahodha wa Kagera Sugar, George Kavila, amesema ametenga muda wa ziada kuhakikisha anaongeza ufiti ili kuwa vizuri zaidi ya ilivyo sasa.
Amesema anajua siku zote mchezo wa fainali unakuwa mgumu hivyo hatowazarau wapinzani wao Mbao hata kama ni timu ndogo, lakini wahakikishe wanatimiza vyema majukumu yao ili kupata taji hilo ambalo kwasasa halina mwenye baada ya Yanga kutolewa.
Banda amesema mbali na ubingwa lakini amekusudia kuonyesha kiwango chake kuwa kipo juu baada yakukaa nje kwa muda mrefu, tangu alipoachiwa huru na kamati hiyo ambayo awali alitakiwa kufungiwa mechi tano bila kucheza.
Mkataba wa Banda na klabu ya Simba unamalizika mwishoni mwa msimu huu na beki huyo amesema hatosaini mkataba mwingine kwasababu tayari kuna timu nchini Afrika Kusini amesaini mkataba wa awali.
ဆင်ဘာ
Stand United
မှတ်ချက် အားလုံး (2)
6-24 06:15