Simba kesho itamtambulisha kiungo wake wa kimataifa Haruna Niyonzima aliyejiunga na timu hiyo akitokea Yanga.

Klabu ya Simba kesho itamtambulisha kiungo wake wa kimataifa Haruna Niyonzima, aliyejiunga na timu hiyo akitokea Yanga.

Kaimu Makamu mwemyekiti wa Simba Iddi Kajuna, amesema taratibu zote za kumtambulisha mchezaji huyo.

"Tupo vizuri maendeleo ya timu yetu yanakwenda sawa huko Afika Kusini na idadi ya wachezaji imezidi kuongezeka baada ya Niyonzima na wale waliokuwa kambi ya timu ya taifa kuongezeka," amesema Kajuna.

Kiongozi huyo ametamba kuwa msimu ujao hawatokuwa na masihara kwani wamekusudia kubeba kila taji ambalo watashiriki.

Amesema wanajivunia ubora wa timy ambayo wameijenga msimu huu na hapana shaka kwamba wanachokitarajia ndi ho watakacho kipata msimu ujao.

Simba bado wapo nchini Afrika Kusini wakijiandaa kwa ajili ya msimu mpya wa ligi ya Vodacom Tanzania Bara.