Kagera Sugar imewasilisha baru ya malalamiko bodi ya ligi wakidai mchezaji wao alionewa

Uongozi wa klabu ya Kagera Sugar umepinga kadi nyekundu aliyoonyeshwa mshambuliaji wao Mbaraka Yusufu, na tayari imewasilisha baru ya malalamiko bodi ya ligi wakidai mchezaji wao alionewa.
Meneja wa Kagera Sugar Mohamed Hussein, ameiambia Goal, mwamuzi hakumtendea haki mchezaji wao kwasababu tukio hilo linaonyesha Yusufu, aliruka kugombea mpira na Kelvin Yondani na siyo kucheza rafu.
“Tumeangalia video na tumejiridhisha kuwa haikuwa halali kwa mshambuliaji wetu kutolewa nje kwa kadi nyekundu hakucheza rafu zaidi ya kugombea mpira na Yondani hivyo tunaiomba bodi ya ligi kuangalia mkanda na kutoa maamuzi,”amesema Hussein.
Kiongozi huyo amesema bali na tukio hilo lakini mwamuzi wa mchezo huo Ngole Mwangole, alionyesha wazi kuwabeba Yanga kwa kutoa kadi nyingi kwa wachezaji wao pasipo sababu za msingi.
Amesema kilicho wauma ni kadi ya mshambuliaji huyo tegemezi ambaye kwasasa ndiyo msaada wao mkubwa hivyo nivyema bodi akajiridhisha na kutengua adhabu hiyo.
“Tumeridhika na matokeo ya uwanjani tumefungwa mabao ya halali kabisa sehemu kubwa ya mchezo mwamuzi alichezesha vizuri lakini kadi nyekundu ndiyo imetupa mashaka,” amesema.
Kama mchezaji huyo hatofutiwa kadi hiyo basi hatoichezea tena Kagera Sugar hadi msimu mechi ya pili ya msimu ujao ukiacha mbili zilizo salia kwenye msimu huu hiyo inatokana na kadi nyekundu ya moja kwa moja aliyopewa jana.
Kagera Sugar
Mbao
Tất cả bình luận