Goal inakuletea washambuliaji bora waliofanya vizuri msimu uliomalizika wa Ligi Kuu

Ligi Kuu Bara imefika tamati wiki mbili zilizo pita, kwa Yanga kuibuka bingwa kwa mara ya tatu mfululizo huku klabu za Simba na Kagera zikikamata nafasi ya pili na ya tatu
Licha ya changamoto ya uhaba wa washambuliaji wazawa wenye uwezo mkubwa wa kucheka na nyavu, ila msimu uliomalizika ulikuwa ni nzuri kwa nyota wazawa hasa mastraika baada ya kufanikiwa kuwafunika Ma-pro kwenye idara ya upachikaji magoli msimu uliopita
Ungana na makala hii Goal inakuletea washambuliaji bora waliofanya vizuri msimu uliomalizika wa Ligi Kuu
Abdulrahman Mussa (RUVU Shooting)
Ndiye kinara wa ufungaji bora Ligi Kuu msimu huu kwa kufumania nyavu mara 13, straika huyu wa RUVU ana sifika kwa uwezo mkubwa wa kufunga katika mazingira tofauti tofauti, ni mtulivu hasa akiwa langoni mwa timu pinzani
Mbaraka Yusuph (Kagera Sugar)
Mbaraka Yusuph amekuwa katika kiwango bora msimu uliomalizika, straika huyo alifanikiwa kumaliza na magoli 12 magoli mawili nyuma dhidi ya kinara wa magoli, kasi yake na uwezo mkubwa wa kufunga kwa mashuti ya mbali kumemfanya kuwa mmoja wa washambuliaji bora msimu uliopita
John Bocco (Azam Fc)
Licha ya majeraha ya mara kwa mara Ila bado Bocco alimaliza na magoli 9 na kuibuka mfungaji bora wa klabu yake, Bocco moja ya silaha yake kubwa ni kuitumia vizuri mipira ya hewani
Rashind Mandawa (Mtibwa Sugar)
Mshambuliaji kutoka kwa Wakata miwa wa Mtibwa, straika huyo amemaliza na magoli 7 kwenye Ligi, Mandawa amefanya vizuri kwa kuiwezesha klabu yake kukamata ndani ya nafasi tano za juu
Ditram Nchimbi (Mbeya City)
Mshambuliaji wa Mbeya City, amemaliza na magoli zaidi ya tano Ligi Kuu, Nchimbi ana sifika kwa nguvu na kuwatoroka walinzi kwenye kutafuta nafasi
森巴
非洲年轻人
阿扎姆
卡盖拉河
全部评论