Ndayiragije amesema anajiona mtu muhimu kwenye timu hiyo baada kuwavua Yanga ubingwa wa Kombe la FA.

Kocha wa Mbao FC raia wa Burundi Ettiene Ndayiragije, amesema anajiona mtu muhimu kwenye timu hiyo baada ya jana kuifunga Yanga na kuwavua ubingwa wa Kombe la FA.
Ndaliyagije ameiaambia Goal, hata kama akiondoka kwenye timu hiyo anaamini ataendelea kukumbukwa kwa tukio la kuifunga timu kubwa ya Yanga na kuwavua ubingwa ikiwa ni timu ya kawaida inayoshiriki ligi ya Vodacom msimu wakwanza.
"Nilipanga kufanya maajabu na nafurahi kuona yametimia hii imeniletea heshima hata nyumbani Burundi ambako nilikuwa naonekana kocha wa kawaida lakini leo kuitoa timu kubwa ya Yanga ambao ndio mabingwa watetezi kumelipaisha juu jina langu," amesema Ndaliyagije.
Kocha huyo aliwapongeza wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata kile alichowaelekeza mazoezini hata kupata ushindi huo.
Amesema baada ya kutinfa fainali sasa wanajipanga kuhakikisha wanashinda mchezo wa fainali dhidi ya Simba na kubeba taji hilo kwa mara ya kwanza.
Amesema hawezi kuwazungumzia wapinzani wao Simba kwa sababu hajajua tarehe ambayo watacheza mechi ya fainali lakini kitu cha muhimu wataendelea kujipanga ili kuhakikisha wana shinda mchezo huo.
Ndaliyagije anajifananisha na kocha wa zamani wa Leicester City Claudio Ranieri ambaye licha ya kutimuliwa kwente timu hiyo lakini ameacha kumbukumbu nzuri ya kuipa timu hiyo taji la ubingwa wa ligi ya Barclays msumu uliopita na mwaka huu imecheza michuano ya UEFA na kufika hatua ya robo fainali.
Young Africans
Mbao
All Comments