Kumekuwapo na taarifa kuwa Yanga ipo kwenye mawindo mazito ya kumvuta kocha huyo kuchukua nafasi ya Juma Mwambusi

Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime, amesema endapo uongozi wa Yanga utaridhia mapendekezo yake, yupo tayari kutua ndani ya klabu hiyo msimu ujao kusaidiana na kocha mkuu George Lwandamina, huku akikazia zaidi mapendekezo yake.
Maxime ameiambia Goal, Yanga ni timu kubwa na yenye maslahi makubwa hivyo hakuna kocha yeyote ambaye itamuhitaji na kugoma kujiunga nayo.
"Siwezi kukataa kwenda Yanga kwasababu soka ndiyo kazi yangu niliyosomea na sikufundishwa kufundisha timu moja, kwaiyo nipo tayari ikiwa yale ninayoyataka nitatimiziwa," amesema Maxime
Hivi karibuni kumekuwapo na taarifa kuwa Yanga ipo kwenye mawindo mazito ya kumvuta kocha huyo kuchukua nafasi ya Juma Mwambusi anayetarajiwa kutupiwa virago.
Mexime amesema bado hajapata taarifa rasmi kutoka ndani ya uongozi wa Yanga, lakini amekiri kuwa, kama Yanga watakubaliana na matakwa yake, kwa maana ya dau analotaka pamoja na vigezo vingine, hatakuwa na tatizo la kutua ndani ya kikosi hicho.
"Mkataba wangu na Kagera Sugar unamalizika mwezi wa saba na sasa tupo kwenye mazungumzo ya kuongeza mkataba mwingine, habari za Yanga kunihitaji nimekuwa nikizisikia tu.
"Siwezi kuweka wazi sana, lakini kikubwa kama wataridhia matakwa yangu sina tatizo lolote kwa sababu kazi yangu haichagui timu, kikubwa ni maelewano, ukiachilia suala la maslahi, vipo vitu vingine lazima vizingatiwe, likiwepo suala la nidhamu kwa wachezaji," alisisitiza Mexime.
Young Africans
Kagera Sugar
All Comments